Peter Crouch alipowasili Liverpool mwaka 2005, alitumia wiki yake ya kwanza hotelini.
Mshambuliaji huyo amekiri kuwa alivutiwa sana na mhudumu wa mapokezi wa hoteli hiyo hali iliyofanya akawaambie wachezaji wenzake.
"Niliwaambia baadhi ya marafiki zangu mazoezini kuwa kuna mwanamke nampenda sana pale Hotelini, ni mzuri sana, Kusema ukweli ni mrembo mno"
Jamie Carragher akawaita wachezaji wengine na kuniambia nirudie nilichokisema:
"Nikarudia nilichokisema nikaongeza kuwa siku nzima namuwaza huyo mrembo, baadae nikaambiwa kuwa mrembo ninayemsifia na kumtaka ni mke wa Xabi Alonso ambae alikuwa ni kuingo mwenzangu wa Liverpool.