Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peter Banda nje mpaka mwakani

Banda Sdfcm Peter Banda nje mpaka mwakani

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema watamkosa mchezaji wao Peter Banda kwa miezi miwili kutokana na kupata majeraha katika mchezo wao wa NBCPL waliocheza dhidi ya Singida Big Star Fc mkoani Singida.

"Mchezo wetu uliopita pale Singida, mchezaji wetu Peter banda alitolewa nje baada ya kupata majeraha na uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa angeweza kukaa nje kwa wiki nne, lakini leo (jana) uchunguzi wa kina umefafanyika na imbeainika atakaa nje kwa zaidi ya miezi miwili.

"Makadirio ni kwamba Peter Banda atarejea uwanjani mwezi Februari wakati michuano ya Kimataifa hatua ya makundi itakapoanza. Kwa hiyo Wanasimba watambue hilo," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live