Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Peter Banda kuikosa Ihefu FC

Peter Banda Kuikosa Ihefu FC Peter Banda kuikosa Ihefu FC

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Malawi Peter Banda amerejea jijini Dar es salaam akitembelea gongo, kufuatia majeraha alioyapata jana Jumatano (Novemba 09), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Stars.

Banda aliyechukua nafasi ya Mkude kipindi cha pili, aliisaidia Simba SC kupata bao la kusawazisha kwa kutumia uwezo binafsi uliopelekea kufunga bao kwa ufundi mkubwa.

Kiungo huyo hakufanikiwa kumaliza salama mchezo huo, kufuatia rafu mbaya aliyofanyiwa na mchezaji wa Singida Big Stars, hali ambayo ilimlazimisha kupelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa matibabu na ndipo alipopatiwa msaada wa gongo la kutembelea.

Banda alisajiliwa Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Nyasa Big Bullet ya nchini kwao Malawi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live