Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pesa za Mo Dewji zimeisaidia Simba - Mangungu

Mangungu Mo Dewji Pesa za Mo Dewji zimeisaidia Simba - Mangungu

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, amesema watu wanaosema uwezekaji hauna faida sio kweli, kwani kabla ya uwekezaji mapato yalikuwa Tsh.Bil. 1.6/=, ambapo baada ya uwekezaji yamepanda hadi Tsh.Bil. 6.9/=, na kwamba imetoka nafasi ya 80 kwa ubora Afrika hadi nafasi ya 7. 

Mangungu ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo, unaofanyika katika ukumbi wa JNICC, uliopo mkoani Dar es Salaam, ambapo pia amesema kuwa pesa ambazo wanachama wa Klabu hiyo walichanga kwa ajili ya ujenzi wa uwanja zilitumika kujenga ukuta wa uwanja wa Bunju ,na pesa zingine zilitumika kuimarisha kambi ya timu hiyo.

"Tujenge Simba imara kwa kizazi cha sasa na baadae. Tuendelee kushirikiana na naamini Mwenyezi Mungu atatutangulia. Mkutano umefunguliwa," alisema Murtaza Mangungu.

Ikumbukwe kuwa, Mohammed Dewji 'Mo Dewji' ndiye mwekezaji wa Simba ambaye kwa mujibu wa makubaliano amewekeza kiasi cha Tsh bilioni 20 ndani ya Wanalunyasi wa mitaa ya Msimbazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live