Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pesa za Mane haziwezi kunibadilisha - mke

Mane Ert Pesa za Mane haziwezi kunibadilisha - mke

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mke wa Sadio Mane, Aisha Tamba amefunguka kuwa pesa na umaarufu wa mwanaume wake huyo si kitu kwake na hazitombadilisha kwa namna yeyote ile.

Aisha mwenye umri wa miaka 18 ameweka wazi hilo kupitia MailOnline "Kwa sasa nipo kwenye maisha mapya najua mambo yatakuwa tofauti lakini sitokuwa na hofu yoyote kwani umaarufu wa Sadio Mane na pesa zake haziwezi kunibalisha jinsi nilivyo".

Aisha meendelea kwa kusema kuwa; "Familia yetu sio watu wa mitandao au kujiachia, nimekulia kwenye mazingira hayo kwa hiyo hakuna kitakachoweza kubadilika baada ya hii ndoa"

Sadio Mane na Aisha walifunga ndoa Januari 7,2024 baada ya ndoa hawakukaa Honey Mood kutokana na msichana huyo kutakiwa kurudi shule kumalizia masomo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live