Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pere kuzikwa makaburi ya ghorofani yaliyovunja rekodi ya Dunia

Kpl Nsn Pere kuzikwa makaburi ya ghorofani yaliyovunja rekodi ya Dunia

Tue, 3 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mwili wa Pele utaanza kuagwa Jumatatu kwenye Uwanja wa Vila Belmiro wa Santos, baada ya shughuli za Luiz Inacio Lula da Silva kuapishwa kuwa Rais wa 39 wa Brazil, juzi Jumapili.

Pele atazikwa leo Jumanne, huku shughuli za mazishi ikielezwa zitafanana na zile za Malkia. Uwanja wa Vila Belmiro, unaotumiwa na Santos FC, timu ambayo Pele alitumikia kwa sehemu kubwa ya maisha ya mpira.

Uwanja huo ndiyo utatumika kwenye shughuli za mazishi Jumatatu na Jumanne. Santos historia yake haielezewi bila ya kumtaja Pele na ndiyo maana wamelichukua jukumu zima la mazishi yake.

Shughuli za mazishi zitadumu kwa saa 24, kuanzia Jumatatu hadi Jumanne, ambapo jeneza lake litapita mitaani na kupita mbele ya nyumba ya “O Rei’s” mama yake, Celeste.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, mama yake Pele amelala tu kitandani na anaripotiwa kuwa na miaka 100.

Kisha mwili wa Pele utakwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya wima, Memorial Necropole Ecumenica. Ni familia tu ndiyo itakayoruhusiwa. Makaburi ya Necropole Ecumenica ni ya ghorofa.

Inaelezwa kwamba makaburi hayo yaliingia kwenye rekodi ya kitabu cha Guinness 1991 kuwa makaburi marefu zaidi duniani yakiwa yamejegwa kwenye jengo la ghorofa 14.

Inaelezwa kwamba mwili wa Pele utapumzishwa kwenye ghorofa ya tisa. Mwanzoni jengo hilo lilijengwa ili kuwa makazi ya watu, kabla ya mwaka 1983 Pepe Altstut kulibadili na kuwa nyumba ya wafu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live