Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Percy Tau aomba radhi kukosa penati

Tau KAAyVRU.png Percy Tau aomba radhi kukosa penati

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Afrika Kusini, Percy Muzi Tau ameomba radhi kwa mashabiki na wapenzi wa soka wa taifa hilo baada ya kukosa penati katika mchezo wao wa AFCON ambapo Mali waliibuka na ushindi wa bao 2-0.

Mchezo huo uliopigwa juzi katika Dimba la Amadou Gon Coulibaly, Tau alikosa penati dakika ya 19 ya mchezo huo na kuupaisha mpira ambapo kipa Djigui Diarra alibaki kuutazama ukitokomea mawinguni.

"Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Afrika Kusini Percy Tau ameomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo kwa kukosa mkwaju wa Pelnaty kweye mchezo wa jana Afrika Kusini dhidi ya Mali mchezo ambao ulitamatika kwa Afrika Kusini kupoteza.

"Afrika Kusini walipata Pelnaty ya mapema kipindi cha kwanza lakini Percy Tau alishindwa kuweka mpira kimiani.

"Hivyo amewaomba radhi na kuahidi mechi zilizosalia kwenye kundi lao watafanya vizuri zaidi ya walivyocheza kwenye mechi yao dhidi ya Mali," amesema Tau.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live