Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep kusalia Man City, hajali adhabu itakayokuja

Pep Guardiola Prefered Arsenal Kocha wa Man City, Pep Guardiola

Sat, 11 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amesema ataendelea kubaki ndani ya klabu hiyo licha ya tuhuma ambazo wanakabiliwa nazo kwasasa klabu hiyo.

Kocha Guardiola amezungumza na wanahabari na kuwashutumu klabu pinzani katika ligi kuu ya Uingereza na kusema kua wapo nyuma ya mashtaka ambayo yanawakabili mpaka sasa, Lakini baada ya kuzugumza hayo alisisitiza kua anataka kuendelea kuwatumikia matajiri hao wa jiji la Manchester.

Kocha huyo anasema vilabu 19 katika ligi hiyo vilikua vinataka klabu ya Manchester City iadhibiwe kipindi ambacho ilishitakiwa kwa kuvunja utaratibu wa matumizi ya fedha na shirikisho la soka barani ulaya, Lakini kocha huyo amesema anaamini kua klabu hiyo haijavunja utaratibu na wataondolewa kwenye mashtaka yao ya sasa.

Kocha Guardiola pia amewakumbusha watu kua wanaihukumu klabu hiyo kwasasa juu ya tuhuma ambazo wanakabiliwa nazo mpaka, Lakini inabidi wajiulize je klabu hiyo ikikutwa haina hatia kama ambavyo wanaeleza malipo yatakua ni yapi kwa upande wao kwani wanazungumzwa kama wameshahukumiwa tayari.

Klabu ya Manchester City inashtumiwa kua na matumizi mabaya ya fedha pamoja kufanya udanganyifu juu ya mikataba ambayo wamekua wakisaini dhidi ya wadhamini wao, Vilevile makocha ambao wamekua wakiwaajiri ndani ya klabu hiyo kitu ambacho kinaweza kuwagharimu kwa kiwango kikubwa ikithibitika ni kweli ju ya tuhuma hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live