Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep kuifundisha England

Tg Pep Guardiola Pep kuifundisha England

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nahodha wa zamani wa Manchester City, Fernandinho amefunguka kwamba kocha wa timu hiyo Pep Guardiola huenda akageukia kufundisha timu za taifa baada ya kuondoka Man City na England inaweza kuwa nchi itakayohitaji kuipata huduma yake.

Fernandinho aliondoka Man City miaka miwili iliyopita baada ya kuhudumu kwa misimu tisa akishinda mataji matano ya Ligi Kuu England, sita ya Carabao na Ngao ya jamii.

Guardiola mwenye umri wa miaka 53, mkataba wake na matajiri hao wa Jiji la Manchester unatarajiwa kumalizika mwaka 2025 na alishawahi kuweka wazi kwamba anafikiria kufundisha timu ya taifa siku moja.

Akizungumza na ESPN, Guardiola alisema: “Ningependa kufundisha timu ya taifa siku moja, aidha kwenye Kombe la Dunia ama Euro, sijajua ni taifa gani litanihitaji nifundishe timu zao kwa sababu ili kupata nafasi ya kufundisha timu ya taifa lazima zikuhitaji kama ilivyo kwenye klabu.”

Guardiola anatajwa kama mmoja kati ya makocha bora kwasasa kutokana na mafanikio aliyopata akiwa na Barcelona, Bayern Munich na Man City.

Kwasasa anapambana kuweka rekodi ya kuingoza Man City kushinda taji la nne mfululizo kwenye Ligi Kuu England baada ya msimu uliopita kuchukua mataji matatu kwa pamoja.

Fernandinho hata hivyo, alikataa kumpa kocha huyo nafasi ya kuifundisha Hispania kwa sababu amekuwa akiunga mkono juhudi za wananchi wa Catalonia wanaohitaji eneo hilo lipewe uhuru wake kutoka kwenye serikali ya Hispania.

“Ni ngumu kusema ataifundisha Brazil ingawa nafasi ipo, sifikirii kuhusu Hispania kutokana na migogoro yao ya kisiasa, lakini naweza kuamini kwamba anaweza akaifundisha England, kwa sababu anawafahamu wachezaji vizuri na kila kitu kuhusu nchi hiyo na pia labda Uholanzi ambako baba yake kwenye mpira wa miguu Johann Cruyff, anatokea,” alisema Fernandinho.

Chanzo: Mwanaspoti