Pep Guardiola alikasirishwa na kanuni mpya ya dakika za majeruhi kujumuisha muda wote ambao mpira utasimama, baada ya Manchester City kufungwa na Arsenal katika mchezo wa Ngao ya Jamii juzi.
Dakika nane za muda wa nyongeza zilikuwa zimeongezwa lakini chini ya kanuni mpya za kupambana na upotevu wa muda mwamuzi Stuart Atwell aliruhusu dakika 14 baada ya Kyle Walker na Thomas Partey kuhitaji matibabu kwa kugongana vichwa.
Baada ya mchezo huo, Guardiola alionyesha kuchoshwa na kanuni mpya:
“Nimeshangaa na itabidi tuzoee, swali zuri kwa bodi, je walishauriana na wachezaji kabla ya kuleta kanuni hizo? Nini maoni yao kwa sababu ndio wanahusika zaidi kwenye hili. Kwa hiyo mechi itakuwa dakika 100? haijawahi kutokea kabisa.” alisema Guardiola.
Naye beki wa Manchester United, Raphael Varane aliandika barua ya malalamiko kwa FIFA kuhusu kanuni hizo mpya akidai hata wachazaji wanastahili kupewa nafasi ya kusikilizwa maoni yao kuhusu hili.