Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep Guardiola kufuata nyayo za Klopp

Pep Guardiola.jpeg Pep Guardiola kufuata nyayo za Klopp

Fri, 2 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Kocha kutoka nchini Hispania Pep Guardiola amesema atazingatia “mambo mengi” kabla ya kuamua kuongeza mkataba wake na klabu yake ya Manchester City.

Kocha huyo ana mkataba Etihad hadi mwaka 2025 na anatazamiwa kuamua kuhusu mustakabali wake baadae mwaka huu.

Guardiola, ambaye aliona mpinzani wake wa karibu Jurgen Klopp akitangaza kuondoka Liverpool wiki iliyopita akitaja ukosefu wa nguvu ya kufanya kazi hiyo, alisema yeye “anajisikia vizuri” lakini anakiri mambo yanaweza kubadilika katika miezi michache ijayo.

“Kwa kawaida uamuzi ni wa baraka,” Guardiola aliuambia mkutano wa wanahabari.

“Hatuwezi kukubali miaka nane ni muda mwingi, mwakani itakuwa misimu tisa, kwa hiyo ni muda mwingi. Ni lazima tuwaone wachezaji, tabia zao zikoje, viwango vyetu, kama tunaweza kuvitunza, na kama wachezaji wanakufuata, ikiwa nimechoka au laa.

“Mambo mengi yanahusika katika hilo. Kuongeza baada ya miaka miwili sio sawa na kuongeza baada ya tisa. Ni tofauti kabisa. Bado nimekaa hapa na niko sawa.

“Nadhani tuna muda sasa najisikia vizuri kama nilivyokuwa siku zote lakini soka linabadilika sana. Nina maoni yangu kwamba unapobakiza mwaka mmoja na nusu kwenye mkataba wako ni mwingi, muda mwingi kwenye soka la dunia.”

City, inayotafuta rekodi ya kutwaa taji la nne la Ligi Kuu ya England mfululizo, imekuwa na kiwango kizuri msimu huu, lakini jana Jumatano ilimenyana na Burnley na kuibuka na ushindi wa 3-1.

Mfululizo huo umejumuisha washindi wa dakika za lala salama dhidi ya Newcastle United na Tottenham Hotspur katika michezo yao miwili iliyopita na wamesalia kwenye nafasi ya kurudia mataji matatu ya msimu uliopita ya Ligi, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la FA.

“Kushinda kunakusaidia kuwa na nguvu zaidi, unapopoteza michezo unakuwa mchovu zaidi,” alisema Guardiola.

“Ninaona timu ikiwa bora na kucheza na wapinzani wagumu kama vile Goodison Park baada ya Klabu bingwa ya dunia au Newcastle au Spurs ugenini na kuona jinsi timu ilivyokuwa, bado tuko pamoja, tuko kwenye njia moja. Hiyo inakupa nishati. Nishati huiwashi wala kuizima.

“Lazima ulete nguvu kila siku na kile unachoishi katika maisha yako ya kibinafsi na mambo mengi. Hiyo ndiyo ninayoishi sasa. Ndiyo maana nilisema mwaka mmoja na nusu ni muda mwingi.”

Chanzo: Dar24