Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep Guardiola aukubali mziki wa Madrid

Pep Guardiola Pep Guardiola aukubali mziki wa Madrid

Wed, 10 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekubali kuwa Real Madrid ni timu bora na ina uzoefu wa kutosha.

Pep amesema hayo baada ya kikosi chake kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Real Madrid jana usiku kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya uliochezwa katika dimba la Santiago Bernabeu.

“Tulipokuwa bora walitufunga bao, walipokuwa bora tuliwafunga bao. Mchezo ulikuwa mgumu mgumu mno. Real Madrid wapo vizuri sana, wana uzoefu na wana timu bora, lakini pia na sisi tupo hivyo,” amesema Pep Guardiola baada ya mchezo.

Kwa upande mwingine Guardiola amesema mchezo wa marudiano wa mkondo wa pili utakaochezwa wiki ijayo Jumatano Mei 18 katika dimba la Etihad utakuwa kama mchezo wa fainali.

Kwenye mchezo wa jana usiku Madrid ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Vinicius Junior dakika ya 36 kabla ya Manchester City kusawazisha kupitia kwa Kevin De Bruyne dakika ya 67.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: