Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pep Guardiola amuonya Jack Grealish

WhatsApp Image 2024 02 28 At 11 .jpeg Pep Guardiola amuonya Jack Grealish

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema Jack Grealish, atarejea kwenye kikosi chake na kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara wakati kiwango chake kitakapoimarika.

Kiungo huyo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 28, alianza mechi 41 akiwa na City katika kampeni ya kushinda mataji matatu msimu uliopita, ikijumuisha fainali za Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Ameanza mechi 19 pekee msimu huu, zikiwamo saba za Ligi Kuu England.

“Ni mchezaji yule yule, ana kocha yule yule, na jinsi tunavyocheza haijabadilika,” alisema Guardiola.

“Ni jinsi tu amefanya. Hiyo ndiyo tofauti.”

Msimu huu, Grealish amekuwa na dakika chache katika Ligi Kuu na kati ya mechi 19 alizoanza, nne alicheza kwenye Ngao ya Jamii, Kombe la Super Cup na mechi zote mbili Kombe la Klabu Bingwa Dunia nchini Saudi Arabia.

Mara ya mwisho alianza mchezo wa ligi Desemba 30, mwaka jana dhidi ya Sheffield United, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na chipukizi Oscar Bobb baada ya dakika 52.

Mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 100 alibaki kwenye benchi wakati wote wa ushindi dhidi ya Bournemouth Jumamosi (Februari 24) na hakuwa na uhakika wa kucheza mechi ya raundi ya tano ya Kombe la FA huko Luton jana Jumanne (Februari 27).

“Nilisema tangu siku ya kwanza, tunamhitaji,” alisema Guardiola.

“Ana ubora maalum kwa timu yetu. Lakini inategemea na yeye mwenyewe. Ninatumaini anaweza kufanya vema.”

Grealish si mchezaji wa kwanza kujikuta ndani na nje ya kikosi cha Guardiola, hayo ni matakwa ambayo kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich ameweka kwa wachezaji wake.

“Siwezi kuwapa wachezaji mechi tatu au nne ili kupata mdundo wao,” aliongeza Guardiola. “Lazima watafute mdundo wa kucheza kwa dakika 20 au 90.

“Katika kiwango cha juu, timu haisubiri kuwa fiti. Huwezi kumpa mtu michezo mitatu au minne ili awe fiti, vipi wale 10 ambao hawachezi wanastahili kutocheza?

“Lazima uone vipindi vya mazoezi na maelezo yote. Wachezaji wanapaswa kujiridhisha kuwa wanastahili kucheza.”

Chanzo: Dar24