Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola ameomba radhi kutokana na kauli aliyoitoa siku chache zilizopita kuhusu nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool Steven Gerrard.
Kocha Guardiola alizungumza kua kuteleza kwa Gerrard katika msimu wa 2013/14 ambapo ilipelekea City kua bingwa haikua kosa la Manchester City, Kocha huyo alizungumza hayo wakati akitetea klabu yake juu ya makosa zaidi ya 100 yanayoikabli klabu hiyo juu ya ukiukwaji wa matumizi ya fedha.
Nahodha Steven Gerrard aliteleza katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Chelsea na kumruhusu Demba Ba kufunga bao ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Liverpool kufungwa mabao mawili kwa bila, Hivo kupelekea klabu ya Manchester City kutwaa ubingwa msimu wa 2013/14.
Guardiola wakati anazungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo wao dhidi ya Arsenal kesho jumatano na kusema “Naomba radhi kwa Gerrard kwa maoni yangu yaliokua hayana ulazima na kijinga niliyoyasema kwa mara ya mwisho kuhusu yeye, Anajua jinsi gani namkubali yeye na kazi yake, Najua amefanya nini kwa nchi hii ninayoshi na kufanya mazoezi, kwakweli najionea aibu kwakua hastahili”
Pep Guardiola licha ya kuomba msamaha mbele ya waandishi wa habari leo, Lakini pia ameweka wazi aliongea na Gerrard na kumuomba msamaha kwakua anajua alimkosea heshima nahodha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool ambae amefanya makubwa ndani ya klabu hiyo pamoja na soka la Uingereza kwa ujumla.