Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amewapongeza wachezaji wake kutokana na kiwango walichokionesha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Liverpool na kufanikiwa kupata alama tatu na kusema ni ushindi bora zaidi kwake.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Etihad ukishuhudia Manchester City wakigawa kipigo kizito kwa Liverpool cha mabao 4-1, Kitu kilichomfanya kuamini namna wamecheza katika mchezo huo basi ushindi huu unakua moja ya ushindi wake bora kabisa katika ukocha.
Kocha huyo anaamini wachezaji wake walicheza vizuri kuanzia dakika ya kwanza hadi dakika 93, Hata pale walipotanguliwa kwa bao moja na Liverpool lakini wao waliendelea kucheza vizuri na ndio sababu iliyowafanya kupata matokeo ya ushindi, Kocha anasema Liverpool nao walikua tishio zaidi hasa walipokua wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.
Kocha Guardiola amemsifu mshambuliaji wake kinda wa kimatifa wa Argentina Julian Alvarez ambae amechukua nafasi ya Earling Haaland ambaye alipata majeraha na kushindwa kucheza mchezo katika mchezo huo, Lakini Alvarez alicheza vizuri na kumkosha kocha wake.
Guardiola pia amempakulia minyama mchezaji wake ghali klabuni hapo ambaye amekua akitupiwa lawama mara kwa mara kwa kudaiwa anacheza chini ya kiwango Jack Grealish, Lakini leo amecheza mchezo mzuri sana dhidi ya Liverpool na kocha wake kusema huyu ndo Grealish ambaye tulimjua.