Kocha mkuu wa Manchester City amebainisha kuwa wakati wote yeye amekuwa akifurahia kuifundisha klabu ya Manchester City.
Pep anasema akiondoka klabuni hapo, hafikirii kufundisha klabu nyingine yeyote England zaidi ya klabu ya Manchester City. Na ikiwa atahitajika England wakati wowote, kurejea kwake kutakuwa ni kwa klabu ya Man City pekee.
Akizungumza na Telegraph, Guardiola amenukuliwa akisema,
“Nikiwa hapa England, siku zote nitakuwa meneja wa Man City, na kama watanitaka nirudi, nitarudi City. Sidhani kama nitafundisha klabu nyingine nchini Uingereza mbali na hii.” – Pep Guardiola
Pep Guardiola ana mkataba wa kuwepo Manchester City hadi 2023 na anaweza kurefusha zaidi mda wake. Bosi huyu Mhispania, mwenye umri wa miaka 50 ameonyesha nia ya kutaka kuwa meneja wa timu ya taifa lakini hana uhakika kuhusu mustakabali wake wa muda mrefu.
Licha ya kutambua kuwa wakati fulani mbeleni, atalazimika kuwa mahali pengine na kuwa na majukumu mengine, pengine na klabu nyingine pia, ana uhakika kuwa hana mpango kuwa atafundisha klabu yeyote ya Preme League mbali na Man City.