Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pengo la Aziz KI linavyoitesa Yanga

Aziz Ki242215 Pengo la Aziz KI linavyoitesa Yanga

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kila timu kuna mchezaji ambaye anakuwa hatari kwenye kutengeneza mashambulizi, yaani uwepo wake uwanjani unaipa timu uwanda mpana wa kutengeneza mashambulizi.

Yanga bila Ki Azizi inafanya vizuri na inatengeneza nafasi pia kama ambavyo tumeona kwenye mechi hizi mbili ambazo mchezaji huyo hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza.

Kwenye mechi zote mbili dhidi ya Kagera sugar na dhidi ya Dodoma jiji Yanga walikuwa wanashambulia lakini wapinzani wao walikuwa wanazuia kwa idadi kubwa ya wachezaji kitu ambacho kilikuwa kinawapa shida Yanga kuwafungua walinzi na timu kiujumla ili kuweza kuweka mpira wavuni.

Ipi faida ya Ki Azizi akiwa uwanjani? Mpinzani anapocheza dhidi ya Yanga akiwa na low block inahitaji uwe na mchezaji anayeweza kuchukua mpira na kuwafata wapinzani huku akiwalazimisha watoke kwenye maeneo yao asilia na kutengeneza spaces ambazo zinaweza kutumika kupata nafasi ya kuweka mpira wavuni.

Ki Azizi anaweza hiyo kazi ya kuwalazimisha wapinzani wamfate kutokana na uhodari wake wa kukaa na mpira tumeona mara nyingi akifanya hivyo na timu inapata matokeo ila kwenye hizi mechi mbili Yanga walishindwa kutengeneza mashambulizi kuanzia katikati waliamua kutumia pembeni kwasababu eneo la kiungo walikuwa wanakutana na wachezaji wengi mno wanaozuia.

Faida nyingine ya Ki Azizi ni uwezo wake wa kupiga mipira iliyokufa kwenye mechi dhidi ya Kagera sugar Yanga walipata mipira mingi iliyokufa tena karibu kabisa na goli lakini hawakutumia vizuri kutokana na kutowepo kwa mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kupiga direct free kick kama Ki Azizi, kwahiyo uwepo wa Ki Azizi pia uwanjani unaipa Yanga tumaini kuwa wakati wowote ikipatikana chance ya free kick huenda wanaweza kupata goli kupitia kwa Ki Azizi.

NB: Wachezaji waliyopo wanafanya vizuri ila nina uhakika Gamondi anatamani Ki Azizi ajiunge na timu aanze kucheza kutokana na hali iliyopo.

Credit: MkazuzuTza

Chanzo: www.tanzaniaweb.live