Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Penati ya dakika za mwisho yawanyima ushindi PSG

FDTPeP6XsAA8NGX Leipzig wakishangilia goli lao la Penati ya dakika za mwishoni

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Ufaransa klabu ya PSG imelazimishwa sare ugenini ya magoli 2-2 na RB Leipzig ya nchini Ujerumani.

Kiungo aliejiunga na PSG akitokea Liverpool, mdachi G.Wijnaldum ndie aliewatanguliza PSG kwa magoli yake mawili dakika za 21 la kusawazisha na 39 lililowapa uongozi PSG na kwenda mapumziko wakiwa kifua mbele.

Wakati lile la kuongoza la Leipzig liliwekwa kimiani na C. Nkunku kabla ya Leipzig kukosa nafasi ya kuongeza goli baada ya kukosa penati iliyopigwa na Silva dakika ya 12 ya mchezo.

Wakati mechi hiyo ya kundi A ikiwa inaelekea ukingoni, Leipzig walipata mkwaju wa penati, mfungaji akiwa ni D. Szoboszlai, na kufanya matokeo kwenda sare ya magoili 2-2.

Man City anaongoza msimamo wa kundi A akiwa na alama 9 akifuatiwa na PSG mwenye alama 8.

Katika mchezo huo PSG walimkosa nyota wao Lionel Messi anaesumbuliwa na majeruhi kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live