Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Penalti ya utata yaibeba Simba kwa KMC

Simbaa Pic Data Penalti ya utata yaibeba Simba kwa KMC

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Ramadhan EliasMore by this Author MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na KMC umemalizika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na wenyeji Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

DAkika 45 za kipindi cha kwanza zilionekana kuwa ngumu kwa timu zote mbili kwani zilimalizika pasi kuwa na bao lolote lililofungwa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kocha wa Simba Sven Vandenbroeck kuwatoa golikipa Aishi Manula na mshambuliaji John Bocco na nafasi zao kuchukuliwa na Beno Kakolanya na Meddie Kagere.

Kwa muda wa dakika nne baada ya kuanza kwa kipindi cha pili lango la KMC lilikua hatarini kwani idadi kubwa ya namba ya wachezaji wa Simba walikua eno hilo wakisaka bao licha ya kuambulia patupu.

Dakika ya 62 makocha wote wawili walifanya mabadiliko KMC Alitoka Mohamed Samata na nafasi yake kuchukuliwa na Kelvin Akijiri wakati kwa Simba alitoka Mzamiru Yassin na nafasi yake kuchukuliwa na Chriss Mugalu.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz