Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Penalti, faulo zinavyoibua vilio Kombe la Dunia Qatar

Penalti Pic Penalti, faulo zinavyoibua vilio Kombe la Dunia Qatar

Tue, 6 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia itafikia kilele leo kwa michezo miwili ambapo wawakilishi wa Afrika, Morocco watapambana na jirani zao Hispania kuanzia saa 12.00 jioni na baadaye saa nne, Ureno itakipiga na Uswisi.

Najua kuna watu watajiuliza kwa nini nimesema Morocco na Hispania ni majirani. Kwa wale waliofika Morocco hasa mji wa Rabat wanajua namaanisha nini. Ni umbali wa kilomita 762.8 na kutokana na ukaribu huo, hakuna tofauti ya saa kati ya Morocco na Hispania.

Ni mwendo wa saa 1 na dakika 27 pamoja na muda wa kuruka na kutua. Kwa kifupi ni karibu. Naweza kueleza mengi kati ya nchi hizo, lakini acha niendelee na mada mahsusi ya kolamu hii. Ni wazi kuwa mpaka sasa nchi kibao zimefungishwa virago katika mashindano haya na kubaki chache, na leo mbili zitatolewa kutokana na mfumo wa mtoano.

Baadhi ya nchi au timu zimelalamika kuhusiana na uamuzi mbalimbali hatua ya makundi na ile ya 16 bora.

Leo tutaangalia baadhi ya matukio makubwa ambayo VAR au Semi Automated Offside Technology (SAOT yamehusika tangu kuanza kwa michuano. Mpaka sasa matukio 22 yamehusishwa na VAR ambapo mawili yalikatakiwa. Kati ya matukio hayo, sita yalizaa mabao ambapo yaliyokataliwa ni tisa huku penalti zilizotokana na VAR ni nane na penalti tano wachezaji walikosa.

Penalti zilizotokana na rafu za kukumbatia ni mbili, kushika mbili ambapo penalti ambayo ilifutwa ni moja na kukataliwa ni mbili.

VAR mpaka sasa imekataa mabao manane kutokana na kuzidi ambapo yaliyokubaliwa kutokana na wafungaji kudhaniwa wamezidi ni mawili. VAR mpaka sasa imesababisha kadi nyekundu moja.

Ghana 0-2 Uruguay

VAR ilibatilisha faulo ambayo awali ilionekana kuwa ni penalti katika tukio lililowahusisha wachezaji wawili Darwin Nunez wa Uruguay na beki wa Ghana, Daniel Amartey. Tukio hilo lilitokea dakika ya 58 ya mchezo ambapo mwamuzi alionyesha ishara ya penalti baada ya Amartey kumzuia Nunez. Hata hivyo, baada ya kuangalia VAR alibadilisha uamuzi wa awali na kusababisha mashabiki na wachezaji wa Uruguay kulalamika.

Hii ilikuwa mara ya pili kwenye mchezo huo ambapo mwamuzi Daniel Siebert alikwama katika uamuzi wa awali pamoja na kufanya marejeo kupitia televisheni iliyopo pembezoni mwa uwanja.

Katika mechi ya Denmark dhidi ya Tunisia, mwamuzi aliona faulo lakini wakati wa kufanya mapitio kama kuna uwezekano wa penalti iliyokana na mchezaji kushika alitoa uamuzi tofauti. Siebert alifanya marejeo ya tukio kwa muda mrefu na hatimaye akahitimisha hakuwa na kosa na kuruhusu mchezo kuendelea.

Ni wazi kuwa Amartey aliupata mpira, lakini swali ni kama kabla ya kuupata alimfanyia faulo Nunez au la...!

Baadhi ya picha za marejeo kutoka pande tofauti za kamera za televisheni zilionyesha beki huyo alimchezea rafu kwanza Nunez na baadaye kuupata mpira tofauti na uamuzi wa VAR. Maoni yamekuwa mengi na wengine walibisha kwamba lilipaswa kuwa penalti lakini uamuzi na mtazamo wa mwamuzi utasimamia maono yake. Mbali ya tukio hilo ambalo lililamikiwa sana, Uruguay walikuwa na madai mengine ya kupata penalti dakika za majeruhi wakati Edinson Cavani alipoangushwa na mchezaji wa Ghana, Alidu Seidu.

Hii ni sawa na dai la penalti la Canada dhidi ya Ubelgiji, ambapo Richie Laryea alipozozana na Axel Witsel na uamuzi wa VAR au waamuzi kutofautiana. Ni aina ya changamoto ambazo huachwa kwenye uamuzi ikiwa mwamuzi ametoa adhabu au la. Penati kwa kosa la Rochet dhidi ya Mohammed Kudus

VAR: Penalti, Ayew akosa

Uamuzi ulikuwa rahisi pamoja na kuzingirwa na matukio mawili tofauti.

Kabla ya uamuzi huo, mashabiki wengi walihoji kwa nini Andrew Ayew hakuhukumiwa aliotea kabla pamoja na kuwa hakuugusa mpira. Wengi walidhani kitendo cha Ayew kutougusa mpira haikuwa sababu ya kutohukumiwa kuwa ameotea kwani alihusika kwa njia nyingine na alifanya kosa.

Hata hivyo, teknolojia ya kuotea ya Fifa (SAOT) ilionyesha alikuwa pembeni ya beki Mathias Olivera, hivyo kibendera cha mwamuzi msaidizi kuwa aliotea hakikuwa sahihi na kubatilisha uamuzi huo.

Baada ya uamuzi huo, suala lililofuata ni kitendo cha kipa wa Uruguay, Rochet dhidi ya Kudus. Ni wazi kuwa Kudus aliupata mpira kabla ya kipa kugongana naye na VAR kuamuru kuwa ni penalti. Uamuzi huo ulikuwa sahihi hata kama mpira ulikuwa unatoka nje.

Japan 2-1 Hispania

Hii ndiyo mechi ambayo ilizua utata na mpaka sasa bado Ujerumani na mashabiki wake wanalalamikia bao la pili la Japan.

Hoja zimekuwa nyingi pamoja na Fifa kutoa ufafanuzi, mbali ya ule wa VAR. Nini kiliotokea? Japan walifunga bao la pili dakika ya 51 dhidi ya Hispania kupitia kwa Ao Tanaka. Bao hilo lilizua utata kwani baadhi ya picha za video na vyanzo mbalimbali vya kamera zilionyesha kabla ya kufunga mpira ulikuwa umetoka nje pamoja na Mitoma kuurejesha mchezoni na kusababisha kupatikana kwa bao.

Tukio hilo lilimfanya mwamuzi kusubiri uamuzi wa VAR ambao ilikubali bao. Sehemu moja ya mpira ulikuwa katika mstari na haukutoka wote. Muhimu hapa siyo tu kuhusu mpira kugusa ardhi, bali hata mviringo unaoning’inia kwenye mstari pia huhesabiwa. Picha zilizopigwa kwa juu zilionyesha mpira huo upo ndani na hakutoka nje wakati zile za pembeni zilionyesha mpira ulikuwa nje. Kamera ya goli ilitumika kufanya uamuzi, lakini picha mbalimbali ziliachwa kukisia juu ya ushahidi uliotumika kuthibitisha mpira ulikuwa bado unachezwa.

Chanzo: Mwanaspoti