Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pedri, De Jong wamuumiza kichwa Xavi Barcelona

Pedri X De Jong Pedri, De Jong wamuumiza kichwa Xavi Barcelona

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Barcelona Xavi Hernandezx ameonyesha kuvunjika sana moyo wakati akitoa taarifa ya wachezaji wake waliopata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Athlec Club, Pedri na Frenkie de Jong huku wakipata sare 0-0.

De Jong alilazimika kutolewa uwanjani katikati ya kipindi cha kwanza akiwa na tatizo la kifundo cha mguu, huku Pedri akitolewa nje kabla ya muda wa mapumziko kwa kile kilionekana kama jeraha la paja.

Hiki ndicho alichosema Xavi baada ya mchezo:

"Majeraha ya Pedri na De Jong hayaonekani kuwa mazuri," aliwaambia wanahabari.

"Tuna huzuni juu ya kukosekana kwao.

Matamshi ya Xavi yanaonyesha kwamba wachezaji wote wawili watakosa mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli mnamo Machi 12 ambayo itakuwa pigo kubwa.

Xavi pia alizungumza kuhusu sare iliyochezwa San Mames baada ya kuhisi kupoteza kwa wachezaji hao wawili kumeathiri uchezaji wa timu yake.

"Labda majeraha yaliathiri timu sana lakini katika kipindi cha pili tukiwa na Lamine tulitengeneza nafasi lakini haikuwa mechi yetu leo," aliongeza.

"Hatukucheza vizuri. Hatuwezi kuwa na furaha leo kwa sababu tunahitaji kufanya zaidi. Kila mtu, mimi kama kocha, wachezaji tunahitaji kuboresha.

Barcelona wana siku chache kabla ya kuwakaribisha Real Mallorca siku ya Ijumaa. Mallorca wanaingia kwenye mchezo wakiwa safi baada ya kuifunga Girona 1-0 Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live