Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pazia Ligi Kuu Bara kufungwa leo

Simba, Yanga Warejea Ligi Kuu Wikiendi Hii Pazia Ligi Kuu Bara kufungwa leo

Tue, 28 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara inafikia tamati leo kwa nyasi za viwanja nane kuwaka moto, licha ya kujulikana bingwa wa msimu huu lakini vita vikali vipo kutafuta mshindi wa pili katika ya Azam FC na Simba.

Michezo ya leo ni mabingwa wapya wa msimu huu Yanga, kukamilisha ratiba dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi. Simba watawakaribisha JKT Tanzania Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Mechi zingine ni Geita Gold FC wakiwa nyumbani Uwanja wa Nyankumbu akimkaribisha Azam FC, Namungo FC dhidi ya Tabora United, Majaliwa Stadium, Lindi, Singida Fountain Gate FC dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba.

Coastal Union dhidi ya KMC FC, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Mashujaa FC watakuwa nyumbani ikiwakaribisha Dodoma Jiji FC. Lake Tanganyika, Kigoma na Ihefu FC dhidi ya Mtibwa Sugar ambaye tayari ameshuka daraja.

Katika michezo ya leo kuna kuwania nafasi ya pili lakini vita vikali ipo katika kuwania tuzo ya ufungaji bora kati ya viungo washambuliaji wawili Stephen Aziz Ki wa Yanga na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wote wakiwa wamefunga mabao 18.

Lakini kuna timu ambazo zinajinasua kushuka na kutafuta nafasi ya kucheza Play Off ambapo Geita Gold FC ambao wako nafasi ya 15 ya pili kutoka chini anakutana na Azam FC ambayo nayo ipo katika vita vya kutafuta nafasi ya pili ili kwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Matumaini ya Simba kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao yamebebwa na Geita Gold FC ambaye akimfunga Azam FC, anaenda kucheza Play Off na kuwapa nafasi timu ya Wekundu wa Msimbazi kwenda kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa.

Kuelekea mchezo huo Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda, alisema maandalizi ya mchezo wa leo upo vizuri na muhimu kwao kupata matokeo ya ushindi.

“Naweza kesho (leo), ndio tunafunga shule kwa sababu tunamaliza mechi ya mwisho wa kumaliza ligi ni muhimu kwetu kushinda na kufikia malengo yetu, mechi hii ni ya maamuzi na kila mmoja ana mahitaji yake. Itakuwa mechi inayohitaji umakini na dakika 90 tutapata uamuzi.

Licha ya kufanya vizuri lakini wachezaji wangu wapo vizuri kisaikolojia na wanafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa leo,” alisema Mgunda.

Kocha Msaidizi George Mketo alisema wamejiandaa kwa mchezo wa leo wanaimani utakuwa mchezo mgumu kulingana na mahitaji ya kila timu kwa upande wao kupata matokeo mazuri.

Alisema wafahamu ubora wa Simba hasa katika maeneo ya pembeni na kati kwa kuwa na nguvu na wanaenda kupambana kutafuta matokeo chanya na kupata alama.

“Simba ina wachezaji wakubwa na wakomavu na tunaenda kucheza kwa namna mbili kukabilian na ubora wa wapinzani wetu na kufanikiwa kuvuna alama muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusalia katika ligi,” alisema Mketo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi alisema wachezaji wako vizuri na wapo tayari kwa mchezo huo, wanacheza kwa tahadhari kubwa kwa sababu ya ubora wa mpinzani wao.

Alisema hakuna siri yoyote zaidi ya wachezaji kupambana na mashabiki wao kuwaunga mkono katika kila hali na anaimani ya kufanya vizuri katika michezo miwili iliyosalia leo dhidi ya Tanzania Prisons na fainali ya Kombe la Shirikisho la CRBD Bank dhidi ya Azam FC.

“Tumefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons, wachezaji wanatambua tunahitaji nini katika mchezo wetu wa leo, kuna baadhi ya nyota nitawakosa akiwamo Jonas Mkude,” alisema kocha huyo.

Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Ahmad Ally, alisema wanafahamu wanakutana na timu bora. Wamefanikiwa kuwaona Yanga walipocheza na Tabora United kwa kuona ubora wao.

“Ili uwe bora lazima ukamfunge aliyekuwa bora, ninawaheshimu na kuwapa nafasi wao na kucheza mpira kwa umakini na kuwapa presha, tunajua uhitaji wa hii mechi na sasa ligi imekuwa mgumu hasa nani anayecheza play off.

Ukiangalia msimamo unaona hakuna mwenye uhakika wa kubaki kwenye ligi kulingana na mtu anayeshika nafasi ya tano anaweza kuporomoka hadi chini asipokuwa makini katika mchezo huu wa leo, tunahitaji kupambana kutafuta matokeo mazuri,” alisema Ahmad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live