Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pauni 40 milioni kumng’oa Jhon Duran Aston Villa

Skysports Jhon Duran Aston Villa 6269819 Pauni 40 milioni kumng’oa Jhon Duran Aston Villa

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aston Villa inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kwa timu yoyote itakayohitaji huduma ya straika wao raia wa Colombia, Jhon Duran, katika dirisha hili.

Chelsea ni miongoni mwa timu zinazomhitaji Duran ambaye tangu ajiunge na Villa Januari mwaka jana amecheza mechi tatu tu za Ligi Kuu England.

KOCHA mpya wa Fenerbahce, mbwatukaji Jose Mourinho amependekeza jina la kiungo wa Tottenham na Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg, 28, ambaye anataka asajiliwe katika dirisha hili.

Mourinho anadaiwa kuwa shabiki mkubwa wa staa huyu ambaye aliwahi kumfundisha alipokuwa kocha wa Tottenham.

Hojbjerg mwenyewe amekuwa akihusishwa kutaka kuondoka kwa muda mrefu kwa sababu hapati nafasi.

REAL Madrid sasa inataka kuwekeza nguvu kwenye usajili wa mastaa wengine inaohitaji kuwasajili katika dirisha hili ikiwa pamoja na beki wa pembeni wa Bayern Munich na Canada, Alphonso Davies, 23, baada ya kufanikisha dili la Kylian Mbappe ambaye ndio alikuwa akiwashughulisha.

Awali, ilielezwa kwamba Madrid ilikuwa ikitaka kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao ili kumsajili Davies.

ARSENAL inakumbana na changamoto kwenye mchakato wao wa kumsajili straika wa Sporting Lisbon na Sweden, Viktor Gyokeres, 26, katika dirisha hili baada ya timu hiyo kudaiwa kwamba inahitaji zaidi ya Euro 80 milioni.

Kiasi hicho cha pesa ndio kinaonekana kuwa kikwazo kwa Arsenal ambayo inahitaji kumsajili kwa pesa isiyozidi Euro 50 milioni.

BORUSSIA Dortimund haina mpango wa kumuongeza mkataba mpya beki wao Mats Hummels, na imempa ruhusa ya kuondoka katika dirisha hili.

Staa huyu wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miak 35, anafuata nyayo za mkongwe mwenzake Marco Reus ambaye anadaiwa kuwa atajiunga na moja ya timu huko Marekani. Mkataba wake wa unameisha msimu huu.

TOTTENHAM, Aston Villa na West Ham zote zinatarajiwa kuwasilisha ofa kwenda AS Roma kwa ajili ya kumsajili straika wa timu hiyo Tammy Abraham, 26, katika dirisha hili.

Tammy ambaye hakupata nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha Roma anataka kurudi tena England ili kujipanga upya baada ya kuona mambo yanazidi kuwa magumu.

CHELSEA na PSG zinatajwa kuchuana katika mbio za kuiwania saini ya straika Mreno Rafael Leao (25) huku ada ya kuvunjia mkataba wake ya Pauni 150 milioni ikitajwa kuwa kikwazo. Na sasa gwiji wa AC Milan, Zlatan Ibrahimovic ameibuka na kusema kwamba Leao, kipa Mike Maignan, na beki wa kushoto Theo Hernandez wote watabaki.

Chanzo: Mwanaspoti