Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paulsen, kocha mpya Stars

F1e68329feaa82822dcd9ea959957ab0 Paulsen, kocha mpya Stars

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Kim Paulsen, raia wa Denmark kuwa kocha wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Mario Ndimbo, imesema kocha huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Taifa Stars, ambayo kwa sasa inawania nafasi ya kucheza Fainali za AFCON, Kombe la Dunia la 2022.

Paulsen aliwahi kuinoa Taifa Stars kati ya 2012 na 2013 ambapo kabla ya kupewa nafasi hiyo alikuwa kocha wa timu za Taifa za vijana.

Kocha huyo anachukua nafasi ya Etienne Ndayiragije aliyefungashiwa virago baada ya kuifundisha timu hiyo tangu Julai 2019.

Chanzo: habarileo.co.tz