Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paul Pogba amshitaki kaka yake Mathias Pogba kwa utapeli

Pogba One Two.jpeg Pogba na kaka yake

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mathias Pogba ameshtakiwa kwa kosa la utapeli dhidi ya ndugu yake, Paul Pogba. Atabaki Mahabusu kusubiri uamuzi wa Mahakama

Paul Pogba aliwasilisha malalamiko akidai kulengwa na utapeli wa Tsh. Bilioni 30.

Uamuzi huu umekuja ikiwa ni siku chache tangu Mathias Pogba akamatwe kwa kuhusishwa na utapeli dhidi ya ndugu yake Paul Pogba. Ataendelea kuwa mahabusu akisubiri uamuzi wa Mahakama kuhusu dhamana yake.

Taarifa za Mahakama zimesema watu wengine wanne pia wamewekwa chini ya uchunguzi rasmi kwa kuhusika na genge la uhalifu dhidi ya nyota huyo wa Juventus.

Mathias amekiri kuhusika na video iliyomuonesha akiahidi kufichua maovu ya Paul Pogba ambaye amewasilisha malalamiko kwa waendesha mashitaka wa Turin akidai alikuwa mlengwa wa njama za utapeli wa Tsh. Bilioni 30.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live