Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patrick Rweyemamu arejeshwa Simba, aifuata timu Misri

Patrick Rweyemamu.jpeg Patrick Rweyemamu na Imani Kajula

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba umemrejesha kikosini Patrick Rweyemamu kuendelea na majukumu yake ya kuwa meneja wa timu hiyo.

Rweyemamu anarudi kwenye nafasi hiyo baada ya msimu uliopita kuondolewa na kuwa Mkuu wa Programu za Soka la Vijana wa klabu hiyo.

Kurejea kwake anachukua nafasi ya Mikael Igendia raiya wa Kenya ambaye alikuwa meneja wa timu hiyo na mkuu wa Sayansi ya michezo.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimeliambia Mwanaspoti, kuwa ni kweli wameamua kumrejesha Rweyemamu ndani ya timu hiyo na keana 'leo jioni' amesafili kwenda Misri kwaajili ya kuungana na timu.

"Rweyemamu leo 'jana' amesafiri kuelekea Misri tayari kwaajili ya kuendelea na majukumu yake ndani ya timu yetu ambayo inaendelea kujiweka fiti tayari kwa msimu mpya," alisema mtoa taarifa huyo na kuongeza." Alisema mtoa taarifa huyo.

Rweyemamu mbali na kushika nafasi tofauti za uongozi ndani ya klabu ya Simba, aliwahi pia kuwa mjumbe wa kamati mbalimbali ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hasa zile zinazohusu soka la vijana.

Mwanaspoti lilipomtafuta Rweyemamu kwaajili ya kuthibitisha taarifa hizo alisema suala hilo kama linaukweli wowote taarifa itatolewa na klabu ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live