Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patrice Motsepe: Msimu ujao tutakuwa na timu 24, Yanga imo?

Patrice Motsepe AFL.jpeg Rais wa Shirikisho la soka Afrika (CAF), Patrick Motsepe

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Patrice Motsepe amethibitisha kuwa msimu ujao Mashindano ya African Football League yatahusisha vilabu 24.

Akizungumza katika mkutano wake na waandishi wa habari hii leo Motsepe amesema;

"Msimu ujao tutakuwa na timu 24 kwenye michuano ya African Football League tutazipata kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio yake katika ligi za nyumbani,"

Msaimu wa ufunguzi wa Mashindano ya African Football League unafunguliwa leo Oktoba 20 katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Simba vs Ahly.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live