Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Patrice Evra atupwa jela mwaka mmoja

Evra Atupwa Jela Patrice Evra atupwa jela mwaka mmoja

Mon, 15 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa zamani wa Man United na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Patrice Evra (43) amehukumiwa miezi 12 kwenda jela kwa kosa la kutelekeza Familia yake nchini Ufaransa.

Evra ambaye alitamba akiwa katika kikosi cha Man United 2006-2014, amepewa adhabu hiyo baada ya kutotoa matunzo ya Watoto wake wawili Lenny na Maona na aliyekuwa Mkewe Sandra Evra kati ya kipindi cha May 1, 2021 hadi September 28, 2023, hata hivyo wawili hao waliachana 2020.

Patrice Evra anadaiwa takribani euro milioni 1 (Tsh bilioni 2.9) ambazo ni malimbikizo ya matunzo ya Watoto, hata hivyo Evra amekata rufaa na kupinga maamuzi hayo kwa madai kuwa hajatelekeza Familia amempa nyumba yenye swimming pool na kumuachia euro milioni 2 (Tsh bilioni 5.8).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live