Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pato: Ballon D'or yangu ni mke wangu

Pato.jpeg Alexander Pato na mke wake

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa zamani wa AC Milan Alexandre Pato anasema familia yake ndio kitu kinachompa furaha zaidi na mpira haujawahi kumpa furaha kama watu wengi wanavyofikiri na kuhusu Ballon D’Or , yeye anamuhesabu mke wake kama tuzo .

“Kadri unavyokua mkubwa ndio unatambua ni nini kinafanya uwe na furaha !”

“Wakati naondoka nyumbani, nilifikiri soka lilikuwa na kila kitu nilichotaka , nilikwenda Italia, Uingereza, Hispania, China huko kote niliteseka, nililia, nilipata maumivu na kote nilikuwa mpweke “

“Pengine sikuwa mchezaji bora zaidi duniani lakini wacha nikuambie kitu,nina amani sana na familia yangu na nafsi yangu “

“Nina mke ninayempenda sana anafanya nijione ni mwenye Ballon d'Or nyingi na kama maisha ni mchezo, basi nimeshinda kila kitu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live