Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Passport kikwazo Biashara United kuelekea Djibouti

Biashara United 123 Kikosi cha Biashara United kikifanya mazoezi siku ya jumanne Septemba

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Bishara united (wanajeshi wa mpakani) wameshindwa kusafiri siku ya Jumatano kuelekea Djibout kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Biashara ni miongoni mwa timu nne ambazo zitaiwakilisha tanzania katika michuano ya kimataifa msimu huu.

Biashara inacheza mechi yake siku ya Ijumaa Septemba 10 majira ya jioni, kwa mujibu wa taarifa waliyoitoa awali ni kuwa wangeondoka hapa nchini siku ya Jumatano Sepetemba 8.

Sasa taarifa za uhakika zinasema Timu ya Biashara na viongozi wake walikwama kusafiri kutokana na ukosefu wa Passport ya kusafiria kwa wachezaji wake.

Taarifa za ndani zinadai wataondoka leo Alasiri, watapitia Ethiopia kisa Djibout na wanatarajia kufika kesho Alfajiri.

Na jioni ya siku hiyo wanatakiwa kucheza mechi yao dhidi ya mwenyeji FC Dikhil majira ya saa tisa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live