Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pascal Wawa amzungumzia Mayele

Mayele X Pascal Pascal Wawa amzungumzia Mayele

Wed, 5 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa Singida Big Stars, Pascal Serge Wawa ameweka wazi mmoja wa washambuliaji ambao anawaona wana kitu kikubwa kwenye Ligi Kuu ni Fiston Mayele anayecheza Young Africans.

Wawa amesema Mayele ni mshambuliaji ambaye kama beki unapokutana naye inabidi utumie akili kubwa kukabiliana naye kwa sababu amekamilika anapokuwa ndani ya uwanja akiitetea timu yake.

“Mayele ni mchezaji mwenye nguvu, spidi na analijua sana goli kwa hiyo kwenye kukabiliana naye lazima uwe na kitu cha ziada, ni mchezaji mzuri sana kwa washambuliaji ambao wapo kwenye ligi hapa,”

“Namwombea kwa Mungu aendelee kufanya vizuri atoke pale alipo na aende sehemu ambayo ataendelea kupata pesa nyingi ili familia yake izidi kujivunia kuhusu yeye.” alisema Wawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live