Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Partey kupigwa bei kisa Mbrazil

Partey Kusepa Arsenal Partey kupigwa bei kisa Mbrazil

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Inaripotiwa kuwa Arsenal itawaweka sokoni Thomas Partey na Jorginho katika dirisha dogo la usajili, Januari ili iweze kusajili kiungo mpya.

Partey amecheza mechi tano tu za Arsenal katika mashindano tofauti msimu huu huku Jorginho akicheza mechi tisa za timu hiyo.

Na jina ambalo linapewa kipaumbele kwa sasa ni kiungo wa Fluminense ya Brazil, Andre ambaye ameonekana kuwa na kiwango bora kinachovutia klabu nyingi Ulaya kuwania saini yake.

Partey na Jorginho wameonekana kuwa na nafasi finyu ya kucheza msimu huu kutokana na uwepo wa Declan Rice aliyenunuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha wakati wa usajili wa majira ya kiangazi huku akianza vyema ndani ya timu hiyo.

Na kiungo Andre mwenye umri wa miaka 22 ndio anaonekana kuichanganya zaidi Arsenal ikipania kumnasa mapema ili asichukuliwe na wapinzani wake.

Liverpool ndio timu inayoonekana kuwa tishio zaidi kwa Arsenal katika vita ya kumuwania kiungo huyo wa Fluminense ikiripotiwa wametenga kiasi kikubwa cha fedha ili wamnase.

Mpango wa Liverpool ulianza tangu wakati wa usajili wa majira ya kiangazi lakini ofa yao ilikuwa miongoni mwa zile zilizokataliwa na Fluminense.

Kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarkt, kiungo Andre kwa sasa ana thamani inayokadiriwa kufikia Euro 15 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti