Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Parlour: Maddison, Ben White wanafaa kuanza England

Ben X Mdisson Maddison na Ben White

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa Arsenal Ray Parlour amemtaka Gareth Southgate kuwaanzisha wachezaji wawili ambao wapo kwenye kiwango kizuri mpaka sasa ambao ni Ben White wa Arsenal na James Maddison wa Leicester City kwenye mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dunia dhidi ya Iran.

Akizungumza na LiveScore, mtangazaji huyo alichagua safu yake kuelekea mechi hiyo , huku beki wa Gunners, Ben White na mchezaji wa Leicester Maddison wakipigiwa chapuo kubwa la kuanza kwenye mchezo huo.

Parlour ambae ana miaka 49, alisema: “Natumai Gareth ataenda na mabeki wanne nyuma dhidi ya Iran. Ningempanga Jordan Pickford katika goli, huku Kieran Trippier na Luke Shaw wakiwa mabeki wa pembeni.”

Aliongezea kwa kusema kuwa; “Kwangu mimi, John Stones lazima acheze katikati, lakini Gareth ana uamuzi mkubwa wa kufanya na nani anayecheza karibu naye.”

Harry Maguire amekuwa na wakati mgumu, na ikiwa hachezi mara kwa mara, ni vigumu kuwa na kasi ushindani wa mchezo, huku akiendelea kusisitiza kuwa kama angekuwa yeye angecheza kamari kwa kuanza na White.

White amekuwa na mchango kwa Arsenal, mara nyingi akicheza nje ya nafasi lakini hajawahi kuwaangusha kwani mchezaji huyo yupo katika hali nzuri, ana kasi na anategemewa sana katikati ya safu ya ulinzi pia.

Katika safu ya kiungo, nadhani unapaswa kujaribu kumleta Maddison. Tena, ni mchezaji mzuri, mwenye kujiamini na kufunga mabao, pia anasema angewachezesha Declan Rice, Jude Bellingham huku Maddison akiwa mbele yao katika safu ya kiungo.

Parlour anasema mbele angemueka Harry Kane, kisha anagemchukua Phil Foden na Bukayo Saka. Kwa upande wa Raheem Sterling amesema hampingi lakini amelinganisha kiwango cha Saka cha hivi karibuni na Raheem, lazima uchague vijana wenye uchu na utulivu kuelekea mechi hizi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live