Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Paredi la ubingwa lasimamisha shughuli mjini Leverkusen

Baye Liv Paredi la ubingwa lasimamisha shughuli mjini Leverkusen

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji na mashabiki wa Bayer Leverkusen wamesherehekea katika mitaa mbalimbali mjini Leverkusen mwishoni mwa juma baada ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu soka Ujerumani Bundesliga na Kombe la Shirikisho DFB-Pokal.

Maelfu ya mashabiki waliojawa na furaha walimiminika barabarani, huku baadhi yao wakifanikiwa kuligusa Kombe la DFB-pokal, walipoungana na vijana wa Xabi Alonso wakati wa msafara na shamrashamra za kusherehekea ubingwa.

"Binafsi, nimefarijika mno hasa baada ya kuwa shabiki wa Leverkusen tangu mwaka 1988 na kila wakati tukisubiri kushinda kombe. Na sasa, hatimaye hilo limetokea. Tunajivunia," ameeleza mmoja wa mashabiki wa Leverkusen.

Kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso amesema, "Najivua sana kuwa na wachezaji na mashabiki hawa. Wajua, siamini kama msimu umekamilika, msimu huu umekuwa kama ndoto. Hali imekuwa nzuri mpaka siku ya mwisho, ni kitu cha kufurahia, nguvu waliotupa mashabiki katika uwanja huu. Nafurahi sana kuwa na kikosi imara kama hiki."

Bayer Leverkusen ilimaliza msimu wa Bundesliga bila ya kupoteza mechi hata moja kwa kujikusanyia alama 90 na kumaliza alama 17 mbele ya Stuttgart iliyomaliza katika nafasi ya pili na Bayern Munich, ambao ni mabingwa kwa misimu 11 iliyopita, ilitulia katika nafasi ya tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live