Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Parade la Yanga latikisa Ulaya

Yanga Paradesz Parade la Yanga latikisa Ulaya

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unaambiwa baada ya video za Paredi la Ubingwa wa Yanga kusambaa duniani kote hivi karibuni zimezua gumzo huko nchini uingereza, ambapo hii ni mara baada ya Shabiki Maarufu wa Klabu ya Arsenal (#Welbeast) kuchapisha moja ya video hizo kwenye ukurasa wake wa X (maarufu kama Twitter) akionesha kushangazwa na kuwapongeza mashabiki wa Yanga kwa namna walivyojitokeza kwa wingi kusherehekea Ubingwa huo.

Baada ya Welbeast kuichapisha video hiyo kurasa mbalimbali maarufu za mashabiki wa vilabu vikubwa ulaya kama UnitedFaithfuls ilikuja na kuandika maoni ndani ya chapishohilo huku wakiwaponda wapinzani wao Manchester City kwamba Parade la Yanga ni bora kuliko hata walilofanya Man City huku wengine pia wakiwaponda Arsenal kwamba Yanga imechukua ubingwa kabla ya Arsenal.

Je, Unadhani ni kweli Yanga wamewafunika Man City?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live