Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Parade la Mabingwa wa nchi, usipime

Yanga Rtesss Parade la Mabingwa wa nchi, usipime

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni June 13, 2023 ambapo Mabingwa wa misimu yote Young Africans tayari wameshawasili Dar es Salaam wakitokea Mkoani Tanga katika fainali za kombe la Azam Federation Cup 2022/2023 ambapo Yanga walibuka na ubingwa baada ya kuifunga Azam goli moja kwa bila (1-0) katika uwanja wa Mkwakwani



Sasa haya ni Mapokezi ya Wananchi waliojitokeza kuwapokea Mabingwa hao kwenye jiji hili la Chalamila huku zikiambatana vibes na shangwe la milele.

Yanga wameandika rekodi nyingine ya kuchukua kombe la Shirikisho la Azam Sports katika fainali iliyochezwa jana Juni 12, 2023 Mkoani Tanga katika Dimba la Mkwakwani baada ya kuibuka kwa ushindi wa goli moja dhidi ya Azam FC.

Shrehe hizo zimehudhuriwa na mashabiki, wanachama na wapenzi wa timu hiyo kuungana nao katika viunga majira asubuhi saa tatu Karume- Msimbazi kisha kumalizika katika Makao Makuu ya Young Africans SC Jangwani Dar es Salaam.

Parade hiyo ya Mabingwa wa kihistoria imesindikizwa na msanii na mmiliki wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz ambae amewaimbia na kuwachezea mashabiki wa Young Africans watakaofika Jangwani Makao Makuu Dar es Salaam.

Katika Msimu huu, yanga wameweka rekodi ambayo haijawahi kutokea nchini kwa kufanikiwa kushinda taji la Ngao ya Jamii, Ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC, Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live