Senegal ipo katika hatihati ya kumkosa kiungo wake Pape Gueye katika mchezo wake wa hatua ya 16 bora dhidi ya wenyeji Ivory Coast, Jumatatu baada ya nyota huyo kukosa mazoezi ya juzi kutokana na majeraha.
Mchezaji huyo wa Marseille ya Ufaransa, alilazimika kutolewa nje ya uwanja katika mechi ya mwisho ya hatua ya makundi dhidi ya Guinea ambayo timu yake iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Jopo la madaktari wa Senegal bado linaendelea na tathmini ya kitabibu juu ya ukubwa wa majeraha ya Pape Gueye ili kuona kama kiungo huyo anaweza kuiwahi mechi dhidi ya Ivory Coast au hatoweza ili kulipa benchi la ufundi fursa ya kufanya uamuzi wa mwisho.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Senegal kwenye mechi za hatua ya makundi ambapo alifunga bao moja huku akicheza katika mechi zote tatu.
Kama kiungo huyo atashindwa kupona kwa wakati, pengo lake linaweza kuzibwa na ama Cheikhou Kouyate, Nampalys Mendy au Idrissa Gana Gueye.
Wakati wakiwa katika wasiwasi wa kutokuwa na Pape Gueye kwenye atua ya 16 bora, timu hiyo imepata auheni kutokana na urejeo wa beki wake Youssouf Sabaly ambaye alikosa mechi tatu za makundi kutokana na majeraha.
Sabaly ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi na kocha Aliou Cisse amefichua kuwa anaweza kumtumia katika mechi hiyo dhidi ya Ivory Coast,