Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga lahamia Simba Queens, wamtema Kocha

Kocha Simba Queens Panga lahamia Simba Queens, wamtema Kocha

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba wameendelea kupiga panga baadhi ya benchi lake la ufundi ambapo jioni hii, wametangaza kuachana na aliyekuwa Kocha wa Simba Queens, Charles Lukula.

Simba wametangaza jioni hii ya Juni 15, 2023 kupitia ukurasa wao wa Instagram.

"Tunamshukuru Charles Lukula kwa kuwa Kocha Mkuu wa Simba Queensc kwa kipindi cha msimu mmoja. Tunamtakia kila la kheri katika maisha yake."

Awali Simba walitangaza kuachana na Kocha wa Makipa Zakaria Chlouha, Kocha wa Viungo Kelvin Mandla pamoja na mchua misuli Fareed Cassiem.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live