Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga laanza kupita Azam FC, Mastaa watatu watemwa

Kangwa Muguna.jpeg Panga laondoka na Mastaa watatu Azam FC

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imeachana na nyota wake watatu wa kigeni, beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola.

Taarifa ya Azam FC kuachana na wachezaji hao imetoka muda mfupi baada ya taarifa ya awali ya kuwaondoa makocha wake wawili, Kocha wa makipa Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.

Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watanaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live