Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga la Mgunda Simba kuondoka na watano

Panga Simba Pic Panga la Mgunda Simba kuondoka na watano

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati mabosi wa Simba wakiwa kwenye harakati za kuboresha kikosi chao dirisha hili dogo la usajili kuna wachezaji watatu hadi sasa ni suala la muda tu kutua ndani ya timu hiyo.

Kama ambavyo Mwanaspoti lilikujuza kwenye matoleo yake ya nyuma na wengine wakafuata upepo nyota hao, Saidi Ntibazonkiza na Kelvin Nashon wote kutokea Geita Gold pamoja na straika anayecheza kwa mkopo Najran ya Saudi Arabia, Kwame Opoku.

Inaelezwa mabosi hao wa Simba kwenye kipindi cha usajili wamepanga kushusha mashine mpya si chini ya tano kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwenye maeneo tofauti kulingana na mapungufu ya mzunguko wa kwanza.

Simba ina nafasi moja ya kusajili mchezaji wa kigeni hadi wakati huu iliyoachwa wazi na mshambuliaji raia wa Serbia Dejan Georgijevic aliyetimka ndani ya kikosi hicho mapema kwenye mzunguko wa kwanza.

Simba kama itafanikiwa kusajili zaidi ya mchezaji mmoja wa kigeni maana yake wageni waliyopo ndani ya kikosi kwa sasa kuna watakaonyeshwa mlango wa kutoka ili nafasi ipatikane za wapya kuingia.

Kuna nyota kama, Victor Akpan, Nelson Okwa wapo kwenye wakati mgumu na huenda wakaonyeshwa mlango wa kutokea kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Wakati huo huko kuna timu tofauti kwenye Ligi Kuu Bara zinampango wa kutuma maombi ya kuwaomba wachezaji wa Simba kwa mkopo kama, Kibu Denis, Nassoro Kapama, Jimsony Mwanuke na wengineo.

Wachezaji hao huenda wakaombwa kwa mkopo kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho cha Simba katika michezo mfululizo.

Chanzo: Mwanaspoti