Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga a Man United Kikosini , Harry Maguire hatoboi

Maguire Harry Mm Harry Maguire

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: Tanzaniawe

Manchester United inakwenda kuwa bize dirisha lijalo la usajili kwa kufungulia mlango wa kutokea mastaa wake kibao.

Kocha, Erik ten Hag anataka kuanzisha zama zake mpya huko Old Trafford, hivyo atahitaji kuachana na mastaa kadhaa waliopo kwenye kikosi kwa sasa ili kufungua milango ya wengine wapya kuingia.

Na sambamba na hilo, kocha huyo Mdachi hataki kutibua kanuni za matumizi ya pesa (Financial Fair Play) hivyo atahitaji kuuza mastaa wake kadhaa kupata pesa za kuboresha bajeti yake ya usajili ili awe kwenye kiwango sahihi cha matumizi.

Na kwenye hilo, kuna wachezaji wapatao 13 waliopo kwenye kikosi cha Man United kwa sasa, watawekwa sokoni kupigwa bei kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, kwa mujibu wa Daily Mail.

Kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi, Man United imelenga kufanya usajili straika mpya, kiungo mpya, beki wa kati mpya, beki wa kulia mpya pamoja na kipa mpya. Hivyo, kuuza baadhi ya wachezaji waliopo hakukwepeki.

Kwa mujibu wa ripoti zinafichua kwamba, nahodha wa miamba hiyo, Harry Maguire ni mmoja wa mastaa hao watakaowekwa sokoni kwa ajili ya kupigwa bei kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Beki wa kati huyo mwingereza, mwenye umri wa miaka 30, amepoteza nafasi kwenye kikosi cha Ten Hag, lakini kwenye mchezo wa wikiendi iliyopita wa Ligi Kuu England, beki huyo ghali duniani, alianzishwa kwenye ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Everton uwanjani Old Trafford.

Anthony Martial, Donny van de Beek, Aaron Wan-Bissaka na Brandon Williams ni wachezaji wengine ambao hatima zao zipo kwenye mashaka makubwa na kwamba ni miongoni mwa watakaopigwa bei. Martial amekuwa akisumbuliwa sana na majeruhi msimu huu, huku Van de Beek naye akiwa nje ya uwanja tangu alipoumia goti Januari mwaka huu.

Beki wa kulia Wan-Bissaka ni mchezaji mwingine aliyeshindwa kumshawishi Ten Hag ili kupata nafasi kwenye kikosi chake.

Kingine ni kwamba kuna klabu zisizopungua 12 zimekuwa kwenye vita ya kumsaka mshambuliaji Anthony Elanga.

Elanga, 20, ameanzishwa mechi tano tu za Ligi Kuu England msimu huu na inaelezwa mwenyewe yupo tayari kuhama.

Alex Telles na Eric Bailly, ambao kwa sasa wapo nje kwa mkopo, nao wanaofunguliwa mlango wa kutokea kwa haki tu. Majina mengine yanayohusishwa na mpango huo wa kupigwa bei kwenye dirisha lijalo ni mabeki Victor Lindelof na Phil Jones.

Na ripoti ya gazeti la Manchester Evening News zinafichua kwamba kocha Ten Hag amepoteza matumaini na winga Mwingereza, Jadon Sancho - ambaye kwenye mchezo uliopita dhidi ya Everton, aliasisti bao la kwanza lilifungwa na kiungo Scott McTominay kwenye ushindi wa mabao 2-0, ambapo bao la pili liliwekwa nyavuni na Martial.

Kipa namba moja, David De Gea bado hajasaini mkataba mpya, akigomea ofa ya klabu inayomtaka ashushe mshahara wake ili aendelee kubaki kwenye kikosi hicho. Mabosi wa Man United bado wanaamini De Gea atakubali ofa mpya na kubaki.

Kuhusu kiungo McTominay, Man United hawana haraka ya kumpiga bei, lakini wameweka wazi kama kutakuwa na timu itakayokuwa tayari kuweka mezani Pauni 50 milioni, basi biashara ya kumuuza mchezaji huyo itafanyika.

MECHI ZILIZOBAKI ZA MAN UNITED MSIMU HUU

-Aprili 13 vs Sevilla (nyumbani)

-Aprili 15 vs Nottm Forest (ugenini)

-Aprili 20 vs Sevilla (ugenini)

-Aprili 23 vs Brighton (Wembley)

-Aprili 27 vs Tottenham (ugenini)

-Aprili 30 vs Aston Villa (nyumbani)

-Mei 4 vs Brighton (ugenini)

-Mei 7 vs West Ham (ugenini)

-Mei 13 vs Wolves (nyumbani)

-Mei 20 vs Bournemouth (ugenini)

-Mei 28 vs Fulham (nyumbani)

Chanzo: Tanzaniawe