Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Panga Yanga kupita na mastaa hawa…

Gift Fred Gd Beki wa Yanga, Gift Fred

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ujio wa mchezaji Augustine Okrah katika kikosi cha Yanga unaelezwa unahitimisha maisha ya beki wa kati kutoka Uganda, Gift Fred ambaye tangu asajiliwe hajapata nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayoshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara na kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa kundi D pamoja na Al Ahly ya Misri, CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana.

“Kutokana na kanuni ya wachezaji wa kigeni kutakiwa kuwa 12, tunalazimika kumfyeka mmoja kati ya wachezaji ambao wameshindwa kuonyesha uwezo kikosini akiwamo Gift Fred, huyu tutaachana naye wakati tunaendelea kuangalia wengine wa kuwatoa ili kupisha majembe mapya kikosini,” alisema mmoja wa vigogo wa Kamati ya Usajili ya Yanga.

Mbali na Gift wengine wanaoelezwa huenda wakafyekwa katika dirisha dogo mara Yanga itakapomalizana na nyota inayowasaka kwa sasa ni Hafiz Konkoni na Jesus Moloko, mbali na nyota wazawa wanaoelezwa watatolewa kwa mkopo kama Dennis Nkane na Crispin Ngushi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: