Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pan African ni kivumbi leo

Pan African Pan African ni kivumbi leo

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kivumbi cha Championship kinatarajiwa kuendelea kwa wakongwe kazini Pan African watakapowakaribisha FGA Talents.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru, Oktoba 28 kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Nyasi za Uwanja wa Uhuru zitakuwa kwenye kazi saa 10:00 jioni kwa wanaume hao 22 uwanjani kusaka ushindi kwa jasho.

Mchezo wao uliopita ilikuwa ni Oktoba 21 ambapo waligawana pointi mojamoja na Mbeya City Uwanja wa Uhuru.

Kwenye msimamo Pan African ipo nafasi ya 15 ina pointi nne kibindoni huku wapinzani wao wakiwa nafasi ya 12 na pointi nane kibindoni msimu wa 2023/24.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live