Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba yashika tiketi ya Gwambina Ligi Kuu Bara

PAMBA Pamba yashika tiketi ya Gwambina Ligi Kuu Bara

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

BAADA ya juzi kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Transit Camp, Gwambina FC ya jijini Mwanza, inahitaji kupata pointi mbili ili kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Kocha Mkuu wa Gwambina, Novatus Fulgence, alisema jana mechi zote za Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu kwa sababu klabu zote zimejipanga kusaka ushindi na kujiweka mahali salama katika msimamo.

Fulgence alisema kikosi chake kilishindwa kupata ushindi katika mechi hiyo ya juzi kutokana wapinzani wao kutumia makosa waliyofanya na hivyo sasa wanajipanga kuingia tofauti katika mechi inayofuata.

Kocha huyo allisema safu yake ya ulinzi haikuwa vema katika siku ya juzi, lakini bado nafasi ya kutimiza ndoto zao na kupanda daraja ipo pale pale.

"Mechi za Ligi Daraja la Kwanza ni ngumu kuliko mechi za mashindano yote hapa nchini, ukipata pointi tatu, ujue lazime kijacho kikutoke, ila bado nafasi tunayo na tunawaahidi mashabiki wetu, tuko eneo salama," Fulgence alisema.

Alisema wanakwenda kuyafanyia kazi makosa waliyoyabaini kwa wachezaji wake na wanaamini mechi inayofuata watakuwa katika kiwango bora.

"Sasa hivi naenda kutafuta pointi mbili katika mechi zetu tatu zilizobakia, tunahitaji kupambana, kila mchezaji ajitoe ili kufikia malengo, hasa katika mchezo watu dhidi ya Pamba," alisema Fulgence.

Aliongeza wanahitaji matokeo mazuri katika mchezo huo ili kufikia alama ambazo hazitafikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi lao kabla ya kukutana na Rhino Rangers na Mashujaa FC.

Gwambina inaongoza Kundi B ikiwa na ikiwa na pointi 41 ikifuatiwa na Geita Gold Mines yenye pointi 33 wakati Kundi A, Dodoma FC na Ihefu ya Mbeya zenye pointi 39, kabla ya mechi zao za jana zinachuana kusaka nafasi hiyo ya kupanda daraja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live