Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba yapenya Robo Fainali ASFC

Pamba.jpeg Pamba yapenya Robo Fainali ASFC

Thu, 17 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Pamba FC imekuwa timu pekee ya daraja la chini ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.

Mabao ya Pamba, mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Muungano nchini yamefungwa na Makiada Makoli dakika ya 15 na Masunga Malulu dakika ya 77, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na Cleophace Mkandala dakika ya 47.

Timu nyingine zilizofuzu Robo Fainali ni Azam FC iliyoichapa Baga Friends 6-0, Geita Gold iliyoichapa Mbuni FC 1-0, Coastal Union iliyoichapa Mtibwa Sugar 2-0, Kagera Sugar iliyoilaza Namungo FC 1-0, Polisi Tanzania iliyoipiga Tanzania Prisons 2-0 na Yanga SC iliyolaza Biashara United 2-1.

Hatua ya 16 Bora ya ASFC itakamilishwa Saa 1:00 usiku leo kwa mchezo kati ya mabingwa watetezi, Simba SC na Ruvu Shooting Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live