Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba yaoga noti, Makalla ataja kikwazo kupanda Ligi Kuu

Makalla X Pamba Jiji Pamba yaoga noti, Makalla ataja kikwazo kupanda Ligi Kuu

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati timu zikijiandaa na michezo ijayo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ameongeza morali na motisha kwenye timu za Pamba Jiji, Mapinduzi FC na Copco FC kwa kuzipatia Sh2 milioni kila moja.

Hafla ya kukabidhi kitita hicho imefanyika jana Jumatano Januari 17, 2024, katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo na kuhudhuriwa na viongozi na wachezaji wa timu hizo.

Makalla amesema baada ya kuwasili mkoani Mwanza amebaini fitina zilizopo miongoni mwa viongozi wa timu zilizopo mkoani humo kuwa ndiyo kikwazo cha timu hizo kushindwa kupanda Ligi Kuu huku akiwataka viongozi na wanachama wa timu hizo kuacha kukwamishana.

Pia ameahidi kuandaa chakula cha jioni cha wadau na kampuni ligi mbalimbali za mikoa na taifa ili ziache kutembeza bakuli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live