Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba yaiwinda Ken Gold Championship

Ken Pic Data Pamba yaiwinda Ken Gold Championship

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Pazia la Ligi ya Championship msimu wa 2022/2023 litafunguliwa keshokutwa Septemba 17 kwa michezo nane kupigwa huku Pamba ikitamba kuendeleza ushindi dhidi ya Ken Gold ya jijini Mbeya.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi katika Uwanja wa Nyamagana jijini hapa saa 10 jioni ambapo ni msimu wa pili mfululizo kwa Pamba kufungua pazia la Championship dhidi ya Ken Gold nyumbani.

Msimu uliopita Pamba ilifungua msimu Oktoba 2, 2021 dhidi ya Ken Gold katika Uwanja wa CCM Kirumba na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo katika mchezo wa marudiano uliopigwa Februari 6, 2022 Ken Gold walitakata kwa ushindi wa bao 1-0.

Kikosi cha Pamba kimefanya maandalizi yake ya mwisho leo saa 6:30 mchana hadi saa 9 alasiri katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ambapo kesho kitapumzika na keshokutwa kuwakabili Ken Gold.

Mazoezi hayo yameongozwa na Kocha Msaidizi, Steven Matata ambaye amesisitiza wachezaji kuzingatia umakini, kutopoteza muda kwa pasi zisizo na msingi, kasi na kufunga mabao huku akiwa mkali kwa wachezaji waliofanya uzembe na wakati mwingine akilazimika kusimamisha mazoezi na kuelekeza upya.

Akizungumzia mchezo wa Jumamosi, Matata amesema ameridhishwa na namna vijana wake wanavyopokea maelekezo na mbinu mpya lakini akasisitiza kuwa bado kuna vitu havijafanyiwa kazi huku akitamba kuwa ana wachezaji wenye vipaji vikubwa na wazoefu watakaombeba kwenye mchezo wa keshokutwa.

"Ukitazama timu zetu zina mabadiliko ya vikosi wenzetu (Ken Gold) wana wachezaji wapya na sisi tumesajili watu bora wenye vipaji na wana uzoefu wa Ligi Kuu na sasa wamekuja kucheza Championship kwahiyo tutafahamiana kimbinu siku hiyo, kikubwa ni kujiandaa vizuri na mashabiki waje kuiunga mkono timu yao," amesema Matata.

Beki wa timu hiyo, Muarami Issa 'Marcelo', amesema wachezaji wamejiandaa vizuri kuipambania timu hiyo na kuipa ushindi ili itimize malengo yake ya muda mrefu ya kupanda daraja kwenda Ligi Kuu.

Chanzo: Mwanaspoti