Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba katikati ya tanuru la moto ikiivaa Fountain Gate

Pembe Pic Data Pamba katikati ya tanuru la moto ikiivaa Fountain Gate

Sun, 2 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Mwanza. Wakati Pamba ikishuka uwanjani leo kuwakabili Fountain Gate katika mchezo wa ligi daraja la kwanza, timu hiyo inakabiliwa na mtihani mzito katika kupangua hesabu za wapinzani wao Geita Gold, Transit Camp na Kitayosce.

Hadi sasa Pamba wapo nafasi ya tatu kwa pointi 27 sawa na Transit Camp waliopo nafasi ya pili na Kitayosce nafasi ya nne huku Geita Gold wakiwa usukani kwa alama 31.

Iko hivi; timu za Kitayosce na Transit Camp ambazo zitacheza na Pamba katika mechi zilizobaki zitakuwa zikiomba dua kwa mpinzani huyo akwame ili kuendelea kubaki katika nafasi hizo kabla ya kukutana naye.

Kama haitoshi Geita Gold nao ambao wanaongoza kwa sasa, watakuwa wakipiga dua kali kuiombea Pamba kupoteza leo ili kumuacha alama nne ambazo zinaweza kuinufaisha timu hiyo katika safari yao ya kwenda Ligi Kuu.

Kali zaidi nao Fountain Gate wataingia kazini kupigana kufa na kupona kusaka ushindi ili kukwepa dhahama ya kushuka daraja kwani pointi 22 walizonazo katika nafasi ya tano si salama kwao.

Ikumbukwe timu nne za chini katika kundi hilo zitashuka daraja moja kwa moja, ambapo tayari Singida United imeshashushwa na sasa zinasakwa tatu kwenda daraja la pili.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz