Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba Kitayosce nani kupanda Ligi Kuu?

Pamba Pointi Wachezaji wa Pamba

Sun, 7 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kitayosce FC imeshinda mchezo wake wa nyumbani [Aki Hassan Mwinyi Stadium, Tabora] kwa goli 1-0 dhidi ya Mbini FC kutoka Mkoani Arusha.

Matokeo hayo yanaifanya Kitayosce FC kufikisha alama 57 kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza mechi 27 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kupanda Ligi Kuu moja kwa moja kama itamaliza katika nafasi ya pili.

Pamba FC ambayo inapigana vita kali dhidi ya Kitayosce FC kuwania kucheza Ligi Kuu msimu ujao, imepata ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani [Nyamagana, Mwanza] baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi JKT Tanzania ambao ni mabingwa wa Championship 2022|23 na tayari wamepanda Ligi Kuu.

Pamba imefikisha alama 56 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku ikiwa imecheza mechi 27! Pamba na Kitayosce zinatofautiana alama moja pekee huku mchuano wao ukiendelea kuwa mkali kuelekea mwisho wa Ligi.

Kwingineko, KenGold FC imeifunga Copco FC kwa goli 1-0 na kuendelea kujiweka katika nafasi salama ya kubaki kwenye Ligi ya Championship baada ya kufikisha alama 43 sawa na Fountain Gate FC na Mashujaa FC.

MATOKEO MECHI ZA JANA

KENGOLD FC 1-0 COPCO

KITAYOSCE FC 1-0 MBUNI FC

PAMBA FC 1-0 JKT TANZANIA FC

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: