Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pamba Jiji inajilamba tu Championship

Pamba Jiji Fc Sq Kikosi cha timu ya Pamba Jiji

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Pamba Jiji FC ya jijini Mwanza imeendelea kung'ara katika michuano ya Ligi ya Championship baada ya leo Ijumaa Novemba 25, 2023 kuitandika Polisi Tanzania bao 1-0.

Mchezo huo umechezwa kwenye Uwanja wa Ushirika jijini hapa ambapo ilikuwa ya vuta ni kuvute kila timu ikishambulia kwa zamu lango la mpinzani wake lakini kukosa umakini kwa safu za ulinzi ilifanya dakika 45 za kwanza kumalizika bila bao lolote.

Kipindi cha pili Pamba Jiji walionekana kulishambulia lango la Polisi kama nyuki na dakika ya 49 mshambuliaji wao Mudathir Said aliimaliza kazi na kupeleka alama zote tatu Mwanza baada ya kufunga bao kwa shuti kali.

Kocha wa Pamba Jiji, Mbwana Makata amesema licha ya mchezo kuwa mgumu lakini anawapongeza vijana wake kwa kupambana na kuchukua alama zote tatu ambayo ndio ilikuwa malengo yao.

"Mchezo ulikuwa mgumu tumetengeneza nafasi nyingi lakini tukatumia moja sasa tunaenda kujipanga kwa mchezo unaofauta," amesema Makata.

Ameongeza kuwa mwenendo wa timu yake unaridhisha kwa namna vijana wanavyopambana kuhakikisha msimu huu wanakata kiu ya mashabiki wa soka Mwanza ambao muda mrefu hawajaiona timu hiyo ikicheza Ligi Kuu.

Kwa upande wa kocha wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema mchezo ulikuwa mzuri wametengeneza nafasi kadhaa lakini kukosa utulivu katika safu yake ya ushambuliaji umemuangusha sasa anaenda kujipanga na mchezo ujao.

Ushindi huo inaifanya Pamba kusogea hadi nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na 21 nyuma alama moja dhidi ya vigogo wa Ligi hiyo TMA Stars ya Arusha ambayo ina alama 25. Pamba ikiwa imecheza mechi 12.

Pamba pia inaongeza ushindani wa ligi hiyo ambayo awali iikuwa ni ya mikoa miwili Mbeya na Arusha ambapo sasa Mwanza nayo imeingia rasmi ikiwa na jambo lake.

Msimamo wa Ligi hiyo, TMA inaongoza kwa alama 25, Pamba Jiji FC ikifuatiwa alama 24, Ken Gold FC ya tatu kwa alama 23 sawa na Mbeya huku Mbuni FC ikishika nafasi ya tano ikiwa na alama 21.

Chanzo: Mwanaspoti